Saturday, May 31, 2014

HIKI NDICHO KILICHOJIRI HII LEO KWENYE SEMINA YA UJASIRIAMALI,ILIYOKUWA IKIRATIBIWA NA COUNTRY FM-IRINGA!!

Wajasiriamali mkoani iringa wametakiwa kufanya kazi zao kwa bidii na kutoogopa kutangaza bidhaa ama huduma zao kwenye vyombo vya habari kwa kuwa vyombo vcya habari ndiyo mhimili mkuu wa maendeleo kwa nyanja zote.
kauli hiyo imetolewa na mratibu na afisa masoko wa country fm ambayo ndiyo radio mama mkoani hapa bw,Huruma Raymond Mgaya wakati alipokuwa akizungumza na wajasiriamali waliohudhuria semina hiyo iliyokuwa ikifanyika katika ukumbi wa chama cha waalimu mtaa wa wilolesi.
katika kunogesha jambo hilo!bwana Huruma Mgaya ametangaza kutoa ofa ya gharama za matangazo kwa wajasiriamali na wafanya biashara wadogo wadogo mkoani hapa,amesema kuwa kwa sasa wajasiriamali watakua wakitangaza bidhaa zao kwa punguzo la asilimia 75% lengo likiwa ni kuwawezesha kuweza kufanikiwa na kufikia ndoto zao.
Mbali na hilo pia amewatoa wasiwasi wafanyabiashara na wajasiriamali kutokata tamaa na kuhofia usumbufa wa TRA kwani lengo la TRA si kuwakandamiza na nchi kwa ujumla pia inahitaji watu wachapa kazi ili kuliletea taifa maendeleo.
unaweza kutangaza nasi kwa tsh.20,000 pekee kwa wiki nzima kwa kupiga simu za afisa masoko wetu ambazo ni simu no.0717179217
                           0754245862

0 comments:

Recent Posts


Unordered List