Unaambiwa
kuna jamaa mmoja kutoka Nairobi amesababisha baadhi ya shughuli
kusimama kwa saa kadhaa kwenye barabara ya Dedan Kimathi kwa kuamua
kujifunga minyororo kwenye Mnara wa shujaa huyo wa kupigania uhuru wa
Kenya akidai kwamba yeye ni mjukuu wa kimathi ambaye ndiye sanamu yake
iliyowekwa.
Kwenye picha ni maafisa wa Baraza la Jiji la Nairobi waliokuwa
wanamzubaisha ili ajifungue na kushuka chini hata hivyo jamaa amekataa
kujifungua kutoka kwenye Mnara mnara huo anaodai ni wa babu yake.
Ingawa
mpaka sasa jina lake bado halijafahamika ameema kwa sauti kwa walio
kusanyika kwamba hatofungua minyororo hadi pale atakaporuhusiwa
kuzungumza na bi.Mukami Kimathi ambaye ni mke wa kimathi kwa sasa yuko
Kinangop kaonti ya Nyandarua ambapo umbali wake ni saa 4 kutoka Jiji la
Nairobi.
0 comments:
Post a Comment