 |
Wafanyakazi
wa radio country fm wakiwa katika picha ya pamoja walipotembelea kitu
cha watoto wenye ulemavu wa viungo cha SAMBAMBA kilichopo Kitwiru |
 |
Kaimu meneja wa Radio Country fm Chiku Mbilinyi akimkabidhi diwani wa kati ya kitwiru zawadi kwa ajiri ya watoto wenye ulemavu |
 |
kaimu meneja wa radio country fm CHIKU akimkabidhi mratibu wa kituo hicho zawadi kwa ajiri ya watoto wenye ulemavu |
 |
watoto wenye ulemavu wakicheza na walimu ambao uwafundisha na kuwatia moyo |
 |
Zainabu mlimbila mtangazaji wa country fm akiwapa watoto maziwa kuonyesha ishara ya upendo na kuwajari |
 |
mratibu wa kituo cha SAMBAMBA akizungumza kitu kwa wageni walio mtembelea |
 |
kaimu
meneja wa country fm akielezea kitu kilichosababisha mpaka wakaamua
kutembelea watoto wenye ulemavu na kuwataka wananchi watoe ushirikiano
na vituo vinavyolea watoto wa aina hiyo |
 |
picha ya pamoja |
 |
marco akiwa na watoto ambao wanalelewa katika kitu cha SAMBAMBA |
|
|
kayanda mc mwenye koti la suti akimyanyua mtoto ambaye analelewa katika kituo hicho |
 |
watuma
salaam mkoa wa iringa katika picha ya pamoja walipoungana na radio
country fm kutembelea kitu cha kulea watoto wenye ulemavu |
|
 |
kaimu meneja wa country fm Chiku akipokea maelezo kutoka kwa mratibu wakituo hicho |
leo 16/06/2014 ni siku ya mtoto barani
Afrika ,katika kuadhimisha siku hiyo radio country fm iringa
imeadhimisha siku hiyo kwa kutembelea kituo cha kulea watoto wenye
ulemavu wa viungo kiitwacho SAMBAMBA,kilichopo kata ya kitwiru manispaa
ya Iringa.
akizungumza na mtandao hu kaimu meneja
wa Country fm Chiku mbilinyi amesema kuwa lengo la kutembelea kituo
hicho ni kutaka kuihamasisha jamii kuwa wasiwatenge watoto wenye ulemavu
kwa nao wana nafasi kubwa katika jamii ikiwa ni pamoja nakushiriki
katika kupanga na kufanya shughuli mbalimbali za kimaendeleo,aidha pia
amewataka wazazi wenye watoto walemavu wasiwafiche ndani na badala yake
wawatoe ili waweze kusaidiwa kwani kuna ulemavu mwingine ambao unaweza
ukapungua kutokana na kufanya mazoezi ambayo mtoto atapewa na wataalamu
wa mazoezi.
Mratibu wa kitu cha SAMBAMBA
ameushukuru uongozi mzima wa radio country fm pamoja na wasikilizaji
wake kwa kuweza kutambua kazi wanayoifanya na kuitaka jamii iunge mkono
kuwasaidia watoto wenye ulemavu,lakini pia ameeleza changamoto ambazo
wanakutana nazo hasa ni kukosa wataalamu ambao wanaweza kuwajenga watoto
kisaikolojia na kimazoezi ili waweze kuwa wanafuraha muda wote hivyo
ameiomba serikali iwasadie wataalamu katika kituo hicho ambacho ni
muhimu kwa jamii .
0 comments:
Post a Comment