



Na Insp Deodatus Kazinja, PHQ
Jeshi
la Magereza nchini limeingia katika Makubaliano rasmi na Chuo Kikuu
Huria cha Tanzania (OUT) katika kuboresha na kuimarisha ushirikiano kati
ya pande hizo mbili.
Makubaliano
hayo yamefanyika leo Jumatatu 02 Juni, 2014 katika Ukumbi wa Mikutano
wa Baraza la Chuo hicho kilichoko eneo la Biafra Kinondoni Jijini Dar es
salaam.
Akizungumza
na wajumbe mbalimbali kutoka Chuoni hapo, Jeshi la Magereza pamoja na
wanahabari Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Tolly Mbwete amesema kuwa
ushirikiano kati ya Magereza na OUT umekuwepo kwa muda mrefu ila hivi
sasa ni kuuimarisha zaidi kwa kufanya mapitio kwenye maeneo ya
ushirikiano kwa lengo kujumuisha maeneo mengi zaidi.
Ametaja
maeneo yanayokusuduiwa katika makubaliano hayo kuwa ni Mafunzo na
shughuli za utafiti, uandaaji wa mitaala na vifaa vya mafunzo hususani
ni katika suala la urekiebishaji wa wahalifu, utoaji wa elimu kwa umma
kuhusu shughuli zinazofanywa na taasisi hizi mbili, ubadilishanaji wa
nyaraka, vitabu vya rejea na vifaa muhimu vya maktaba, maendelea ya
kitaaluma kwa watumishi wa Jeshi la Magereza na wafungwa nakadhalika.
Kwa
upande wake Kamishna Jenerali wa Magereza John Minja amesema kwa muda
wote Jeshi la Magereza limekuwa tayari kushirikiana na Chuo Kikuu Huria
cha Tanzania kwa kutoa vibali mbalimbali kwa wanafunzi na wakufunzi
wanaotaka kufanya tafiti katika maeneo ya Magereza, kutoa vibali kwa
watumishi wa Jeshi la Magereza kusoma katika chuo hicho na kutoa
ushirikiano wa dhati kwa wafungwa wanaotaka kusoma kwa kutumia chuo
hicho wakiwa gerezani.
Makubaliano
haya ya leo yatakuwa ya msaada sana kwa Jeshi la Magereza katika
kulifanya liwe la kisasa na kulipunguzia matumizi” Alisema Kamishna
Minja.
Katika
hafla ushuhuda wa wafungwa kusoma na kufanikiwa wakiwa gerezani
ulitolewa na ex-mfungwa Haruna Pembe aliyepata shahada ya sheria (LLB)
akiwa gerezani na sasa yuko nje baada ya kushinda rufaa yake akiwa sasa
anafanya shahada ya pili ya sheria katika Chuo Kikuu hicho. (Picha zote
na Insp. Deodatus Kazinja, PHQ)
0 comments:
Post a Comment