Kutokana
na vurugu zilizofanywa na baadhi ya wamachinga jijini Mwanza, ghasia
hizo zimezua sura mpya ya kudai viongozi wa Halmashauri ya jiji kupitia
Chama cha Mapinduzi (CCM) walipokea fedha kutoka katika misikiti mitatu
ili kuwaondoa wafanyabiashara wanaoziba misikiti hiyo.
Katika
jiji la Mwanza leo hali imekuwa shwari isipokuwa eneo moja la
Makoroboi, eneo la misikiti machinga waliovunjiwa vibanda vyao vya
biashara wamekusanyika wakiendelea kutoa madai ya kuwa serikali
inawaonea.
Katibu
mwenezi wa wa CCM wa Mkoa Simoni Mangelepa amekanusha uvumi uliopo kuwa
wafanyabiashara hao wamenyimwa haki ya kufanya biashara katika eneo
lote la Makoroboi .
“Si
kweli kwamba tumewanyima machinga hawa kuuza bidhaa zao katika eneo
lote la Makoroboi bali ni machinga waliozingira eneo la kuabudu iliyoko
misikiti mitatu, niwaombe viongozi wa wamachinga wanapoenda katika vikao
na kukutana na viongozi wa Halmashauri ya jiji, viongozi wa machinga
wasiwapotoshe wamachinga bali wawaelimishe wafanyabiashara wao kuwa
waende katika maeneo waliyopangiwa na halmashauri,” alisema Simoni.
Aidha
ameeleza kuwa Halmashauri ilitenga maeneo 11 kupitia wilaya zote mbili,
wilaya ya Ilemela na Nyamagana kwa ajili ya wamachinga cha ajabu
waligoma kuondoka eneo la misikiti mitatu wanakoabudu Wahindi, maeneo
waliondolewa ni halali Chama cha Mapinduzi kinawapenda wafanyabiashara
wote na kila raia ana haki ya kuabudu kwa uhuru.
Kwa
mijibu wa oparesheni inayoendelea jijini Mwanza kwa ajili ya kuweka mji
safi tangu kuanza Mei 17 hadi kufikia Juni 11 lengo ikiwa ni kusafisha
jiji, mfanyabiashara anapofanya biashara eneo lolote bila kufuata
utaratibu anachukuliwa hatua na serikali, vile vile anakuwa anachafua
mji ndio mana kuna maeneo maalumu ya biashara na kufuata utaratibu wa
halmashauri.
Wamachinga
wanaofuata utaratibu uliopo watafanya shuguli zao kwa amani na
hawatafuatwa na kiongozi yeyote wa serikali, sisi kama serikali
hatuwanyanyasi wamachinga tunatambua kuwa wamekopa mikopo mbalimbali kwa
nia ya biashara na wanapaswa kurejesha hivyo ni vema wakatii sheria na
si kuleta vurugu.
Nitoe
rai kwa viongozi wa machinga na wafanyabiashara ndogondogo wawaelimishe
wafanyabiashara wao kwa kuwaeleza waende katika maeneo waliyopangiwa
ili kuwapisha waumini wa misikiti mitatu waabudu kwa uhuru kama ilivyo
katika madhehebu mengine.
0 comments:
Post a Comment