Thursday, July 24, 2014

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MKUTANO WA 45 WA CPA JIJINI ARUSHA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wajumbe wa Chama cha Wabunge kutoka nchi za Jumuiya ya Madola (CPA) katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC jijini Arusha. Mheshimiwa Makamu wa Rais alifungua mkutano wa 45 wa CPA unaozikutanisha nchi za Afrika unaofanyika nchini Tanzania kuanzia leo Julai 24 hadi Julai 27, 2014. Mkutano huo sambamba na masuala mengine pia unajadili juu ya wajibu wa mabunge na mchango wao katika kusimamia utawala bora pamoja na kusaidia serikali za Afrika kubuni mipango ya maendeleo inayolenga vizazi vya sasa kwa lengo la kuijenga Afrika ijayo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Makamu wa Rais wa CPA na Spika wa Ufalme wa Lethoto, Enoch Sephir Motanyane, wakati akiondoka nje ya ukumbi wa AICC baada ya kufungua rasmi mkutano wa 45 wa CPA unaozikutanisha nchi za Afrika unaofanyika nchini Tanzania, jijini Arusha kuanzia leo Julai 24 hadi Julai 27, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya Wabunge wakati akiondoka nje ya ukumbi wa AICC jijini Arusha baada ya kufungua rasmi mkutano wa 45 wa CPA unaozikutanisha nchi za Afrika unaofanyika nchini Tanzania, kuanzia leo Julai 24 hadi Julai 27, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Spika wa Bunge la Jamhuri, Anne Makinda na Mwenyekiti wa CPA Tawi la Tanzania, Azan Zungu, wakifurahia ngoma ya asili wakati walipokuwa wakiwasili kwenye ukumbi wa AICC, jijini Arusha kufungua mkutano wa 45 wa CPA unaozikutanisha nchi za Afrika unaofanyika nchini Tanzania, kuanzia leo Julai 24 hadi Julai 27, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na wabunge baada ya kufungua rasmi mkutano wa 45 wa CPA unaozikutanisha nchi za Afrika unaofanyika nchini Tanzania, kuanzia leo Julai 24 hadi Julai 27, 2014. Picha na OMR

Jeshi la kanda kupambana na Boko Haram

Mataifa manne ya Afrika Magharibi yameazimia kuunda kikosi cha pamoja ili kukabiliana na kitisho kinachoongezeka cha kundi la itakadi kali za Kiislamu la Boko Haram, linaloendesha shughuli zake hasa nchini Nigeria.

Kila moja ya mataifa hayo ya Nigeria, Niger, Chad na Cameroon, litachangia wanajeshi 700 kwenye kikosi kinachonuwiwa kuboresha mapambano ya kanda hiyo dhidi ya wapiganaji hao.
Mataifa hayo manne yanayopakana na ziwa Chad, eneo ambalo ni ngome ya Boko Haram, tayari yanabadilisha taarifa za kijasusi na yanaratibu kwa pamoja usalama wa mpakani katika eneo, lakini kuunda kikosi cha pamoja chenye ukubwa huu itakuwa hatua kubwa zaidi katika ushirikiano wao.
Tangazo la kuundwa kikosi hicho lilitolewa wakati wa mkutano wa mamawziri wa ulinzi kutoka mataifa hayo manne, lakini hakukuwa na taarifa zaidi juu ya muda au eneo vitakakopelekwa vikosi hivyo. Wapiganaji wa Boko Haram wameua maelfu ya watu tangu mwaka 2009, walipoanzisha juhudi zao za kuunda taifa la Kiislamu nchini Nigeria.
Kiongozi wa Boko Haram Abubakar Shekau. Kiongozi wa Boko Haram Abubakar Shekau.
Raia zaidi wateketezwa
Matukio ya uripuaji mabomu na mashambulizi mengine yamekuwa jambo la kawaida kaskazini mwa Nigeria, lakini Boko Haram ilianza kupamba vichwa vya habari kimataifa miezi iliyopita, baada ya kuwateka wanafunzi zaidi ya 200 kutoka shule mjini Chibok. Utekaji huu ulipelekea kutolewa miito ya kuchukuliwa hatua, na ahadi kutoka kwa marais wa kanda hiyo kuanzisha vita kamili dhidi ya wapiganaji hao.
Niger na Cameron zimeimarisha hasa usalama katika maeneo ya mipakani, lakini hakukuwa na ishara zozote za mashambulizi makubwa yanayovihusisha vikosi vya kanda. Shirika la kutetea haki za binaadamu la Huma Rights Watch lilikadiria wiki iliyopita kuwa wapiganaji hao wameuwa zaidi ya raia 2000 katika nusu ya kwanza ya mwaka huu.
Jana Jumatano, miripuko miwili katika mji wa kaduna, ambayo iliwalenga mhadhiri maarufu wa dini ya Kiislamu na rais wa zamani wa Nigeria, ilisababisha vifo vya watu wasiopungua 42 katika vurugu za hivi karibuni zinazolaumiwa kwa kundi la Boko Haram.
Maandamano ya kutaka kurejeshwa kwa wasicha wa shule. Maandamano ya kutaka kurejeshwa kwa wasicha wa shule.
Gavana Kaduna ahofia jimbo lake
Polisi ilisema shambulio la kwanza lilifanywa na mripuaji wa kujitoa muhanga akiulenga msafara wa Sheikh Dahiru Bauchi, kiongozi wa dini ambaye ameukosoa vibaya uasi wa miaka mitano wa Boko Haram.
Shambulio lingine lililotokea saa mbili baadaye na kuuwa watu 17 lilimlenga Muammadu Buhari, moja wa wapinzani maarufu nchini Nigeria, ambaye pia aliiongoza Nigeria kama dikteta wa kijeshi kuanzia mwaka 1983 hadi 1985.
Gavana wa jimbo la Kaduna Mukhtar Ramalan Yero alitangaza amri ya saa 24 ya kutotembea usiku, na msemaji wake alieleza wasiwasi wa gavana huyo, juu ya kuripuka kwa machafuko katika mji huo maarufu kwa mapigano ya kidini katika miaka ya karibuni, kwa sababu walengwa wote wa mashambulizi hayo, Bauchi na Buhari, wanashikilia nyadhifa muhimu machoni mwa watu.
Mwandishi: Iddi Ismail Ssessanga/afpe,rtre Mhariri: Hamidou Oummilkheir
source:DW

Ndege ya Algeria yatoweka na watu 116

Ndege ya Air Algerie imetoweka ikiwa na abiria 116
Shirika la ndege la Algeria , Air Algerie, limesema kuwa limepoteza mawasiliano na moja ya ndege zake ilipokuwa ikitoka mji mkuu wa Burkina Faso Ouagadougou.
Afisa huyo anasema kuwa ndege hiyoya Air Algerie ilikuwa imepaa dakika 50 katika anga ya Sahara mara ya mwisho mawasiliano yao.
Ndege hiyo iliokuwa inaeelekea mji mkuu wa Algiers, ilikuwa na watu mia na kumi na wahudumu sita .
Oparesheni ya dharura ya kuitafuta ndege hiyo ieanzishwa,
Ndege hiyo nambari AH 5017 inamilikiwa na shirika la ndege la kihispania la Swiftair.
Mwandishi wa BBC Alex Duval Smith aliyeko katika mji mkuu wa Mali Bamako anasema kuwa kuna habari kuwa ndege hiyo huenda ilianguka katika eneo la janga la sahara kati ya
mji wa Gao and Tessalit .
Mwandishi huyo wa BBC ananukuu ripoti kutoka kwa wanajeshi wa kulinda amani walioko huko Mali na duru za shirika la habari la AFP.
Brigadia mkuu wa majeshi ya kulinda amani nchini Mali Koko Essien, amesema kuwa maeneo hayo ya jangwani yana idadi ndogo sana ya wakaazi kwa hivyo ni vigumu kupata habari kutoka huko na inawabidi kutafuta ilikoanguka ndege hiyo.
Ndege ya Air Algerie imetoweka ikiwa na abiria 116
Aidha Brig Essien anasema kuwa eneo hilo linamilikiwa na wapiganaji waasi .
Wamiliki wa ndege hiyo Swiftair wamesema kuwa ndege hiyo aina ya MD83 ilikuwa imeomba kubadili uelekeo wake kutokana na hali mbaya ya anga na ukungu mkubwa karibu na mpaka wa Algiers.
Ndege namba AH 5017 husafiri kupitia njia ya Ouagadougou-Algiers mara nne kwa wiki,AFP imeripoti.
Raia wa Algeria ni miongoni mwa abiria waliokuwa ndani ya Ndege hiyo,Gazeti moja la Algeria limeripoti.
Mwezi Februari ndege ya kijeshi ya Algeria ilianguka na kuuwa watu 77 waliokuwemo.
Tukio hili la hivi punde Linaloongeza wasiwasi kuwa njia inayotumiwa na misafara ya ndege ziendazo sehemu hiyo inapitia eneo lenye utata la anga ya Mali.

Wednesday, July 23, 2014

AJARI YA NDEGE:MIILI KUPELEKWA UHOLANZI

 
Mabaki ya ndege ya Malaysia yakiwa yamezagaa
Kwa mara ya kwanza miili iliyopatikana kutoka kwenye ndege ya Malaysia iliyotunguliwa juma lililopita nchini Ukraine itasafirishwa mpaka nchini Uholanzi kwa ajili ya kutambuliwa.
Uholanzi iko kwenye siku ya maombolezo kwa ajili ya watu 298 waliokufa kwenye ajali hiyo, 193 kati yao raia wa Uholanzi.
Maafisa wa kiintelijensia wa nchini Marekani wamesema waasi wanaoiunga mkono Urusi waliitungua ndege hiyo kimakosa, lakini hakuna viashiria vyovyote kuhusu tukio hilo,vinavyohusiana moja kwa moja na Urusi.
Waasi wameshutumiwa kuwakwamisha wapelelezi kwa kuwapa ushahidi wenye mashaka na kutoa taarifa zisizo sahihi kuhusu idadi ya miili iliyopatikana.
Katika hatua nyingine maafisa wa nchini Malaysia wamekabidhi kisanduku cheusi chenye kurekodi mawasiliano ndani ya ndege kwa mamlaka za uholanzi.

Thursday, July 17, 2014

KAMA HUKUZIONA PICHA ZA ILE AJALI ILIYOTOKEA JANA USIKU NA KUUA WATU WANNE MKOANI IRINGA,CHEKI HAPA!!

Iringa 3
 Lori la Mizigo likiwa limepaki katikati ya kilabu hicho cha pombe ambacho kilisambalatishwa chote na chini ni mabaki ya kilabu hicho.
Tunaomba Radhi kwa Picha
Iringa 1
  Miili minne ya Marehemu ambao walifariki papo hapo baada ya Lori hilo kugonga kilabu hicho ikiwa imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya Rufaa ya Iringa.
 Mashuhuda wakiwa wanashuhudia ajali hiyo baada ya kutokea
 Baadhi ya wananchi wa Eneo la Isimila wakiwa wameongezeka kushuhudia ajali hiyo mbaya iliyo uwa wata watano papo hapo.
 Hivi ndivyo Lori hilo la Mizigo lilivyo umia vibaya baada ya kugonga kirabu hicho na kukisambalatisha usiku wa kuamkia jana na kusababisha vifo vya watu watano papo hapo.
 Baadhi ya Ndugu wa Marehemu wakipata taarifa za Ajali hiyo katika eneo la tukio isimila
Ndugu wa Marehemu wakiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Iringa kwa ajili ya kuwaona Marehem hao.

Picha zote na Iringa Yetu Blog

LOUIS VAN GAAL AWATAFUTIA SHAVU SCHOLES NA NEVILLE MANCHESTER UNITED

Getting his points across: Van Gaal speaks to the media for the first time as Manchester United manager
Van Gaal akizungumza na waandishi wa habari kwa mara ya kwanza katika klabu ya  Manchester United.
Mtabakia: Louis van Gaal amesema atawatafutia kazi Paul Scholes na Phil Neville.
LOUIS van Gaal ameahidi kuwajumuisha Paul Scholes na Phil Neville katika benchi la ufundi la Manchester United.
Mholanzi huyo aliyeanza kazi rasmi United wiki hii amesema atawatafutia kazi ya kufanya katika benchi lake.
Ryan Goggs tayari alishateuliwa kuwa msaidizi wa pili wa Van Gaal na Nicky Butt alibaki kuwa kocha wa timu za vijana.Staying put: Louis van Gaal says he will find roles for Paul Scholes and Phil Neville
Kocha huyo wa zamani wa Uholanzi amethibitisha kuwa Neville na Scholes ambao kwa pamoja walikuwa wachezaji wa kikosi cha mwaka 1992 kilichoshinda kombe la FA, watapatiwa kibarua cha kufanya.
Alisema: "Nicky Butt tayari anatusaidia. Tutatafuta kazi ya Paul Scholes na Phil Neville. Hicho ndicho tunataka".
"Tunatakiwa kurithi ubora wa watu hawa na tutazungumza na kila mtu binafsi na tusubiri na kuona"
The new team: Van Gaal will be assisted by Ryan Giggs
Timu mpya: Van Gaal atasaidiwa na Ryan Giggs

Neville aliletwa Old Trafford na kocha aliyefukuzwa kazi, David Moyes kama msaidizi wake wa timu ya kwanza na alibakishwa baada ya Giggs kuteuliwa kuiongoza Man United kwa muda katika mechi nne za mwisho za msimu uliopita.
Inafahamika kuwa United walitaka kumbakisha Neville kwa pointi kuwa mchezaji huyo wa kikosi cha 1992 ni muhimu katika klabu hiyo, lakini kutokana na ujio wa Van Gaal majukumu ya kocha huyo yanaweza kupunguzwa zaidi ukilinganisha na msimu uliopita

KAMPUNI YA MICROSOFT WORD KUWAFUTA KAZI WAFANYAKAZI 18,OOO/=

microsoftkm 
Kampuni ya kiteknolojia ya Microsoft inatarajia kupunguza takribani ajira elfu 18 za wafanyakazi wake na kuweka rekodi ya kupunguza watu wengi zaidi katika historia ya kampuni hiyo kwa miaka 39.
Punguzo kubwa litafanyika kwa ajira elfu 12 kwa kitengo chake cha Nokia ambacho kampuni hiyo ilinunua mwezi Aprili.
Punguzo hilo ni kubwa tofauti na matarajio ya watu 6000 yaliyokuwepo awali.
Kampuni hiyo inaajiri watu laki moja na 27 dunia nzima ikiwa ni pamoja wa wafanyakazi 3,500 nchini Uingereza.
Kampuni hiyo imekataa kusema ni ajira kiasi gani zitapunguzwa nchini Uingereza ikiwa ni matokeo ya mabadiliko hayo.

Tuesday, July 08, 2014

*AIPS YAANDAA MAFUNZO KWA WANAHABARI CHIPUKIZI



Habari wadau, Chama cha Kimataifa cha Waandishi wa Habari za Michezo (AIPS), kimeandaa mafunzo kwa ajili ya waandishi wa habari za michezo chipukizi wa umri kati ya miaka 19-25 yatakayofanyika Doha Qatar mwishoni mwa mwaka huu wakati wa mashindano ya Dunia ya Mchezo wa Kuogelea.

Kutokana na hali hiyo, AIPS imetoa nafasi chache kwa watakaokidhi vigezo vyao katika mabara mbalimbali duniani. Hivyo nimeattach barua yao na nini kinatakiwa katika mafunzo hayo, ambayo wahusika watagharamia nauli ya kwenda Doha na kurudi mji husika anaotoka mhusika, chakula na malazi muda wote atakaokuwa huko.

Kwa vile hatua ya mwisho itahusisha chama cha nchi husika kumthibitisha muombaji, naomba wote watakaofikiri wana sifa zinazotakiwa wasome vizuri hiyo attachment, kisha watume kwa Makamu Mwenyekiti TASWA, Egbert Mkoko ambaye ndiye atasimamia jambo hilo kwa email: njali5@yahoo.com nataswatz@yahoo.com

Lakini pia kama utamudu unaweza ukaomba binafsi bila kutumia chama na mwisho wa kufanya hivyo ni Agosti 15 mwaka huu na watume kwa email:youngreporters@aipsmedia.com. Kwa watakaotaka kupitia TASWA wajitahidi kabla ya Agosti 10 mwaka huu.

Tusihofie kuomba kwani mwaka 2011 aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mtanzania mwenzetu, Mwita Mwaikenda aliomba nafasi hiyo na aliipata. Ukiwa unahitaji ufafanuzi tuwasiliane 0713-415346.

Nawasilisha,
Katibu Mkuu TASWA

Recent Posts


Unordered List