
Van Gaal akizungumza na waandishi wa habari kwa mara ya kwanza katika klabu ya Manchester United.
Mtabakia: Louis van Gaal amesema atawatafutia kazi Paul Scholes na Phil Neville.
LOUIS van Gaal ameahidi kuwajumuisha Paul Scholes na Phil Neville katika benchi la ufundi la Manchester United.
Mholanzi huyo aliyeanza kazi rasmi United wiki hii amesema atawatafutia kazi ya kufanya katika benchi lake.
Ryan Goggs tayari alishateuliwa kuwa msaidizi wa pili wa Van Gaal na Nicky Butt alibaki kuwa kocha wa timu za vijana.

Kocha
huyo wa zamani wa Uholanzi amethibitisha kuwa Neville na Scholes ambao
kwa pamoja walikuwa wachezaji wa kikosi cha mwaka 1992 kilichoshinda
kombe la FA, watapatiwa kibarua cha kufanya.
Alisema: "Nicky Butt tayari anatusaidia. Tutatafuta kazi ya Paul Scholes na Phil Neville. Hicho ndicho tunataka".
"Tunatakiwa kurithi ubora wa watu hawa na tutazungumza na kila mtu binafsi na tusubiri na kuona"

Timu mpya: Van Gaal atasaidiwa na Ryan Giggs
Neville
aliletwa Old Trafford na kocha aliyefukuzwa kazi, David Moyes kama
msaidizi wake wa timu ya kwanza na alibakishwa baada ya Giggs kuteuliwa
kuiongoza Man United kwa muda katika mechi nne za mwisho za msimu
uliopita.
Inafahamika
kuwa United walitaka kumbakisha Neville kwa pointi kuwa mchezaji huyo
wa kikosi cha 1992 ni muhimu katika klabu hiyo, lakini kutokana na ujio
wa Van Gaal majukumu ya kocha huyo yanaweza kupunguzwa zaidi
ukilinganisha na msimu uliopita
0 comments:
Post a Comment