Askofu mstaafu Desmond Tutu
Askofu mkuu mstaafu wa Cape Town,Desmond Tutu,ameahirisha
mipango ya ziara zake kwa mwaka mzima ujao kutokana na sababu za kiafya.
Taarifa iliyotolewa na taasisi yake imeeleza kuwa Askofu
huyo ataanza matibabu hivi karibuni ili kukabiliana na tezi dume ambayo amedumu
nayo miaka kumi na mitano iliyopita.
Binti wa Askofu huyo amemuelezea baba yake mwenye umri wa miaka themanini na miwili,kwamba hatahudhuria tuzo za Nobel zitakazo fanyika baadaye wiki hii huko Rome, Italia.
0 comments:
Post a Comment