Jajaaaaaa,
mshambuliaji wa Yanga, Jenilson Santos (jaja) akijikunja kupiga mpira
wa krosi mbele ya beki wa Azam fc, Erasto Nyoni, wakati wa mchezo wa
Ngao ya Jamii uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam,
leo jioni.
Katika
mchezo huo Yanga imeibuka na ushindi wa mabao 3-0, huku mabao mawili
yakifungwa na jaja aliyefunga bao la kwanza kwa kuunganisha krosi murua
ya Simon Msuva na la pili akimchungulia kipa wa Azam fc, Mwadini Ali.
Bao
la tatu lilifungwa na Simon Msuva, ambaye alimpiga kanzu kipa Mwadini
Ali na kubaki yeye na goli na kisha kutupia katika nyavu ndogo.
Jaja, akishangilia bao lake la kwanza na kuwaacha wachezaji wa Azam hoi wasijue la kufanya.
Jaja
akishangilia huku mwamuzi wa mchezo huko, akiwa nyuma yake akionekana
kama anamuunga mkono, lakini hapa alikuwa akiwarudisha uwanjani
wachezaji hao.
Wachezaji wa Yanga wakimpongeza mwenzao Jaja baada ya kutupia bao la pili.
Simon Msuva (kushoto) na Mrisho Ngassa, wakimsapoti Jaja kushangilia bao lake kwa kumfundisha kucheza song la mdogo mdogo.
Hilo ndo bao la kwanza la jaja.
Hapa jaja akijaribu kuwatoka mabeki wa Azam fc (msitu).
Jaja, akimfinya beki wa Azam, Agrey Morris.
Jaja akiruka kuwania mpira na beki wa Azam, Himidi Mao.
Jaja
akipewa medali na wachezaji wenzake wakati wakikabidhiwa zawadi yao ya
Ngao ya Hisani baadda ya kuifunga Azam 3-0. HILI NI TOLEO MAALUM LA
KUONYESHA KAZI ALIYOIFANYA MCHEZAJI HUYU ALIYEKUWA AKIBEZWA NA KUZOMEWA
KILA ALIPOKUWA AKIGUSA MPIRA, KWA MATUKIO ZAIDI YA PICHA ZA MCHEZO HUU
ZITAWAJIA BAADAYE, KAA NASI.
0 comments:
Post a Comment