Aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Gabriel Fuime akifikishwa mahakamani wakati wa hatua za awali za kesi hiyo.
Jengo
lililoporomoka Marchi 29, mwaka 2013 katika mtaa wa Indira Gandhi ulioko
katika wilaya ya Ilala, jijijini Dar es salaam na kuua watu 27.
Na Mwene Said wa Globu ya Jamii
MAHAKAMA
Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, imefuta mwenendo wa kesi ya
mauaji iliyofunguliwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini
dhidi aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Gabriel Fuime na
wenzake 11, wanaohusishwa na kuporomoka kwa jingo la ghorofa 16 katika
mtaa wa Indira Gandh na kuua watu 27 badala yake wafunguliwe mashitaka
ya kuua bila kukusudia.
Akisoma
uamuzi huo,Jaji Salvatory Bongole Ijumaa iliyopita baada ya kukubaliana
na hoja zilizowasilishwa mbele yake na mawakili wa upande wa utetezi
kuwa na mashiko ya kisheria. Jaji Bongole aliamuru washtakiwa kuendea
kushitakiwa kwa makosa ya zamani ya kuua bila kukusudia na siyo makosa
ya mauaji.
Alisema
washtakiwa wanastahili kuendelea kuwa nje kwa dhamana zao kama livyokuwa
kabla upande wa Jamhuri kubadilisha hati ya mashitaka yao Marchi 12,
mwaka huu kutoka mauaji ya bila kukusudia na kuwa kesi ya mauaji ya
kukusudia.
Jaji
alitupilia hoja za upande wa Jamhuri ulikuwa ukiongozwa na Wakili wa
Serikali Mkuu, Bernard Kongola kuwa hati ya mashitaka ya mauaji ya
kukusudia iliyowasilishwa mahakamani ilikuwa sahihi na inajitosheleza
kuwawezesha washitakiwa kupanga utetezi wao. Katika uamuzi wake
uliopokelewa kwa shangwe na washitakiwa na ndugu zao waliokuwa
wamefurika katika viunga vya Mahakama Kuu, Jaji Bongole alisema kuwa
kitendo cha kubadilisha mashitaka kutoka mauaji ya bila kukusudia hadi
mauaji ya kukusudia kulifanywa kwa nia mbaya na upande wa Jamhuri.
Alieleza
kuwa upande wa mashitaka ulikuwa na nia ya kuwafanya washtakiwa wabaki
rumande na hii ilidhihilishwa tangu awali pale walipofikishwa kwa mara
ya kwanza kwa kosa la mauaji ya bila kukusudia na upande wa mashitaka
ukapinga dhamana.
Mara
baada ya Mahakama ya Kisutu kuwapa washtakiwa dhamana upande wa Jamhuri
ulikata rufaa kupinga dhamana hiyo. Hata hivyo, Jaji Bongole alifafanua
kuwa upande wa Jamhuri uliachana na rufaa hiyo mara baada ya mwaka mmoja
kupita uliwasilisha Mahakama ya Kisutu maombi ya kubadilisha hati ya
mashitaka ya mauaji ya kukusudia.
“Mabadiliko
haya hayakufanywa kwa nia njema bali yalilenga kuwanyima haki
washtakiwa… Vitendo vya makusudi vya namna hii havikubaliki na vinapaswa
kukoma mara moja,” alisisitiza jaji huyo wakati akisoma uamuzi wa
kuwabadilishia washtakiwa hao hati ya mashitaka.
Mbali na
Fuime, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Razah Ladha (68), Goodluck
Mbaga (35), Wilboard Mugyabuso (42), Mohamed Abdulkari (61), Charles
Ogare (48), Zonazea Oushoudada (60), Vedasto Richale (59), Michael Hemed
(59), Albert Munuo (56), Joseph Ringo (43) na Ibrahim Mohamed.
Katika
kesi ya msingi, upande wa Jamhuri unadai kuwa Marchi 29, mwaka 2013
katika mtaa wa Indira Gandhi ulioko katika wilaya ya Ilala, washtakiwa
hao waliwaua watu 27.
Katika
tukio hilo watu 27 walipoteza maisha wakiwemo Yusuph Khari, Kulwa Alfan,
Hamada Musa, Kessy Manjapa, Hamis Mkomwa, Boniface Bernard, Suhail
Karim, Salman Akbar, Selemani Haji, Selemani Mtego, Sikudhani Mohamed,
Ahmed Milambo na Salum Mapunda.
Wengine
ni Selemani Mnyamani, John Majewa, Mussa Mnyamani, Devid Herman, William
Joakim, Abdulrahaman Mwiha, Emmanuel Christian, Mmanyi Ngadula, Adivai
Desiki, Emmanuel Wahai, Augustino Chuma, Gabriel Godwin Kamwela, Philipo
Kusimula, Betod Mwananengule na Zahda Abbas.
0 comments:
Post a Comment