
Naibu
Waziri wa Maji, Mh. Amos Makalla ameahidi Sh. Milioni 500 kwa ajili ya
utekelezaji wa miradi ya maji kwa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza.
Mhe.
Makalla alitoa kauli hiyo jana, alipotembelea Wilaya hiyo kukagua
utekelezaji wa miradi ya maji na hali ya huduma ya maji wilayani humo.
“Nawapongeza
sana Halmashauri yenu na uongozi wake kwa kununua mashine kwa ajili ya
kuchimba visima vya maji, sijawahi kutembelea Wilaya yoyote nchini
nikakuta jambo hili. Kitendo cha Halmashauri kukusanya mapato yake na
kufanya hivi, mnastahili pongezi na kuwa mfano kwa Halmashauri nyingine
nchini,” alisema Makalla.
“Nimeridhishwa
na jitahada zenu na nitahakikisha mnapata mgao wa Sh. Milioni 500 ili
kufanikisha lengo la kupatia ufumbuzi tatizo la maji Muheza,” aliongeza
Makalla.
Naibu
Waziri alisema kwamba kama kiongozi mwenye dhamana kwenye Serikali Kuu,
atahimiza maamuzi yafanyike upesi ili jitihada zinazofanywa na Wilaya ya
Muheza zifikie lengo walilojiwekea kuwapatia wananchi maji.
Aidha,
Naibu Waziri wa Maji, Mh. Amos Makalla leo ameendelea na ziara yake kwa
kutembelea Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira jijini Tanga (Tanga
UWASA) na kujionea utendaji wa Mamlaka hiyo.
Mhe.
Makalla alisikia taarifa ya utendaji wa Mamlaka hiyo na kufurahishwa
nayo, hasa kwa jinsi walivyofanikiwa kupiga hatua kubwa ya kupunguza
kiwango cha upotevu wa maji kwa kiasi kikubwa na ukusanyaji mzuri wa
mapato kutoka kwa wateja wake.
“Kwa
kweli nimefurahishwa mno na jitihada zenu za kupunguza upotevu wa maji
na kwa kufikia kiasi cha asilimia 23 ni kiwango kizuri, ukilinganisha na
Mamlaka nyingine nchini. Hasa ikizingatiwa hii ni changamoto kubwa na
kama Wizara tunafanya jitahada kupata suluhisho lake,” alisema Makalla.
Pia,
aliongeza ukusanyaji mzuri wa mapato ni hatua kubwa kwa Mamlaka hii,
kwani itarahisisha na kuchangia utendaji mzuri wa kazi na maendeleo ya
Mamlaka hiyo katika kuhakikisha inainua Sekta ya Maji jijini Tanga na
mkoa mzima kwa ujumla.
Katika
ziara hiyo Mhe. Makalla amefanikiwa kutembelea miradi ya maji ya vijiji
vya Misengeni, Mikwamba na Michungwani, wilayani Muheza. Na vilevile,
chanzo cha maji cha Mibayani, kituo cha kusukuma na kutibu majisafi cha
Mowe na eneo la ujenzi wa mabwawa ya majitaka lililopo Utofu, Tanga
Mjini.
Mhe.
Makalla ameanza ziara yake ya siku 6 jana mkoani Tanga, ikiwa ni hatua
ya kuhakikisha utekelezaji wa programu ya wa Big Results Now na miradi
yote ya maji inatekelezwa kwa kasi na ufanisi ili kuleta matokeo yenye
tija na kwa wakati.
0 comments:
Post a Comment