Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius
Likwelile akiwa na ujumbe kutoka mfuko wa maendeleo ya uchumi wa Kuwait
wakisubiri kutiliana saini mkataba wa makubaliano ya kuanzisha mradi wa
maji katika Wilaya ya Same na Mwanga. Aliye kulia kwake ni Bw.
Abdulwahab A. Al- Bader ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo.

Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius
Likwelile akitia saini makubaliano ya mradi wa maji katika Wilaya ya
Same na Mwanga. Aliye kulia kwake Bw. Abdulwahab A. Al- Bader ambaye ni
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa maendeleo ya uchumi wa Kuwait. Waliosimama
nyuma ni Bi. Suzan Mkapa, Mkurugenzi wa sheria kutoka Wizara ya Fedha na
wengine ni wataalam kutoka Kuwait.

Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius
Likwelile na Bw. Abdulwahab A. Al- Bader ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa
Mfuko wa maendeleo ya uchumi wa Kuwait wakibadilishana mikataba hiyo
baada ya kutiliana saini.

Wajumbe
kutoka Tanzania na Kuwait wakishangilia kwa furaha baada kusainiwa kwa
mkataba wa kuanzisha mradi wa maji katika Wilaya ya Same na Mwanga.Picha
zote na Ingiahedi Mduma-Wizara ya Fedha tukiwa Washington DC
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius
Likwelile, mchana wa leo ametiliana saini makubaliano ya mkataba wa
kuanzisha Mradi wa Maji katika Wilaya ya Same na Mwanga. Dr. Likwelile
alisaini Mkataba huo kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Mfuko wa maendeleo ya uchumi wa Kuwait . Aliye wakilisha
Mfuko huo ni Bw. Abdulwahab A. Al- Bader ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa
Mfuko.
Aidha
katika kutiliana saini Mkataba huo Dr. Likwelile alimueleza Bw.
Abdulwahab A. Al- Bader kuwa, Serikali ya Tanzania inatambua kuwa mfuko
umetoa Dola za Kimarekani milioni 34.0 sawa na shilingi Bilioni 56.10 za
Kitanzania kwa ajili ya kusaidia mradi wa maji katika Wilaya ya Same na
Mwanga. Hivyo inatoa shukrani zake za dhati kwa nchi ya Kuwait na hasa
kwa mfuko huu wa maendeleo ya kiuchumi.
“Msaada
huu tulioupata leo utaisaidia Serikali kutatua tatizo la maji katika
wilaya ya Same na Mwanga, hii inaonyesha ni jinsi gani mfuko huu wa
Kuwait unavounga mkono na kutekeleza jukumu zima la kushiriki katika
masuala ya kijamii na ya kiuchumi kwa nchi yetu ya Tanzania, hivyo
tunaomba muendelee kutusaidia”. Alisema Dr. Likwelile.
Dr.
Likwelile alimueleza Bw. Abdulwahab A. Al- Bader kuwa, kama anavyofahamu
gharama za mapendekezo ya mradi mzima ni Dola za Kimarekani million
110.43 na hii inahitaji uchangiaji kutoka katika mifuko mingine kama
BADEA, mfuko wa maendeleo wa Saudia , Mfuko wa Kimataifa wa OPEC na
Serikali kuchangia fedha kusaidia mradi huu. Kwa hili sina wasiwasi nalo
kwani ninafuraha kujua kwamba umeshakubaliana na ninaujasiri kuwa
jitihada zako zitafanikiwa.
“Mradi
huu wa maji wq wilaya ya Same na Mwanga unalenga kusaidia kuwepo kwa
maji kwenye jamii mbalimbali zilizopo kwenye mradi huo.” Aliongeza
Dr.Likwelile.
Aliendelea kusema kuwa,mradi huo utakapo kamilika :
(i) utaongeza kiwango cha watu wengi kuweza kupata maji safi na salama ya kunywa.
(ii)
Uchumi wa Same na Mwanga utaimarika pamoja na hali ya afya kwa jamii
nayo itakuwa imara hasa kwa maeneo yale yanayoguswa na mradi.
(iii) Hali ya maisha ya watu wa Same na Mwanga itainuka.
“Mafanikio
ya ukamilishaji wa mradi huu ni muhimu sana kwa uchumi wa jamii na
maisha bora kwa watu wa wilaya ya Same na Mwanga”. Alisema Likwelile.
Dr.
Likwelilie alimalizia kwa kusema kuwa“Tanzania na Kuwait ni marafiki wa
muda mrefu sana, hivyo tutazidi kushirikiana na kuhakikisha kila kitu
kinaenda sawa”.
Hali ya hewa ya mjini Washington Dc. ni mvua za vipindi na baridi kiasi.
Imetolewa na:
Ingiahedi Mduma
Msemaji
Wizara ya Fedha
Washington D.C
11/10/2014
0 comments:
Post a Comment