Usiku
wa kuamkia Ijumaa iliuwa ni zamu ya Uefa ndogo almaarufu Europa
League. Mechi kadhaa zilirindima katika viwanja mbalimbali na kukonga
nyoyo za wapenda soka.
Tottenham iliialika Besiktas ya Uturuki , hadi mwisho wa mchezo timu hizo zilitoshana nguvu kwa sare ya 1-1.Wakati hayo yakijiri, timu nyingine kutoka Uingereza Everton walikuwa wageni wa FK Krasnodar ya Urusi, matokeo katika mpambano huo ni sare ya bao 1-1.
Villarreal wao waliialika Apollon Limassol ya nchini Cyprus, hadi mwisho wa mchezo huo Villareal wakawaadabisha wapinzani wao kwa jumla ya mabao 4-0.
Celtic wao walikuwa nyumbani kumenyana na Dinamo Zagreb ya Croatia, hadi kipyenga cha mwisho Celtic wakafanikiwa kuondoka na kitita cha pointi tatu baada ya kushinda goli 1-0.
Dynamo Kiev ya Ukrain nayo ikaisambaratisha Steaua Bucharest ya Romania kwa mabao 3-1.
Kwingineko Fiorentina ya Italy ilikuwa ugenini kucheza dhidi ya Dinamo Minsk ya Belarus, hadi dakika tisini za mchezo huo wenyeji Dinamo Minsk ikaangukia pua kwa kufungwa mabao matatu patupu.
FC Zurich wao waliikaribisha Borrussia Monchengladbach /Borrusia Monchinglandbak/ ya nchini Ujerumani, katika mchezo huo hakuna mbabe aliyepatikana huku kila timu ikiambulia pointi moja kibindoni kwa sare ya bao 1-1.
0 comments:
Post a Comment