Gari aina ya Toyota Raum lenye namba za usajili T483 CMU likiwa eneo la kituo cha mabasi.
Tairi likiwa limepasuka baada ya ajali hiyo.
Dereva wa gari lililopata ajali ambaye jina lake halikufahamika mara moja akiongea na simu baada ya kunusurika kifo.
ABIRIA waliokuwa katika kituo cha mabasi eneo la Quality Plaza jijini
Dar wakisubiri usafiri wamenusurika kifo baada ya gari aina ya Toyota
Raum lenye namba za usajili T483 CMU, kuhama njia katika barabara ya
Nyerere na kuparamia kituo hicho.
Dereva wa gari hilo mwenye asili ya Kihindi ambaye jina lake
halikufahamika mara moja alishindwa kulimudu ndipo lilipovuka ukingo
unaotenganisha barabara hiyo na kuhamia upande wa pili kisha kuparamia
kituo cha abiria. Katika ajali hiyo hakuna mtu aliyejeruhiwa.
0 comments:
Post a Comment