Chande
Abdallah na Deogratius Mongela FUNDI ujenzi aliyefahamika kwa jina la
Omari Mkulu (25) amedaiwa kuuawa na kutupwa ndani ya bwawa baada ya
kudaiwa kutoweka nyumbani kwa takriban siku tatu.
Mwili wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Omari Mkulu (25)ambaye alikuwa fundi wa ujenzi.
Tukio
hilo lilitokea maeneo ya Mabwawa Saba, Mabibo jijini Dar ambapo
majirani wa eneo hilo walidai kuwa waliiona maiti ya Omari ikiwa inaelea
kwenye moja ya bwawa eneo hilo lakini kutokana na maiti hiyo kuvimba
haikuwa ikitambulika.
Mmoja wa ndugu wa marehemu Omari Mkulu akilia kwa uchungu.
Kwa
mujibu wa marafiki zake ambao walifanya jitihada za kusafiri hadi
Chanika kwa baba wa marehemu ili kuhakikisha kama kweli maiti ile
ilikuwa ni ya Omari na kuthibitisha kuwa ni kweli, walidai kuwa kabla
marehemu hajatoweka, alilipwa fedha zake za ujenzi ambapo ilidaiwa kuwa
alikwenda kuzitumia kwenye pombe mpaka usiku wa manane.
Bwawa lililopo eneo la Mabibo (Mabwawa Saba) ambapo maiti ya marehemu Omari Mkulu ilikutwa ikielea.
“Siku
ile marehemu alikuwa amelewa sana kwa sababu alikuwa amepata fedha zake
za malipo, tangu siku ile hakuonekana tena mpaka leo hii. Kwa kuwa sura
na mwili wake umevimba tumezitambua nguo zake alizovaa,” alisema mmoja
wa marafiki hao aliyeiomba hifadhi ya jina.
Waandishi
wetu walipofika katika eneo la tukio, waliishuhudia maiti hiyo
ikitolewa kwenye bwawa hilo ambapo umati wa watu waliofika katika eneo
hilo walipewa nafasi ya kumtambua ambapo mmoja wa watu waliofika alidai
kuwa mtu huyo ni jirani yake, akawaelekeza waandishi nyumbani kwa
marehemu.
Marehemu Omari Mkulu (kushoto) akiwa na marafiki zake enzi za uhai wake.
Waandishi
wetu walifika nyumbani kwa marehemu na kuzungumza na mama mkubwa wa
Omari aliyejitambulisha kwa jina la Zainabu Omari ambaye alisimulia kwa
uchungu kuwa mwanaye huyo alitoweka nyumbani Agosti 10, mwaka huu baada
ya kumpatia shilingi 2,000 alizomuomba.
“Siku
hiyo alikuwa na shilingi 5,000 mimi akanipa shilingi 2,000 halafu
akaniambia kuwa jioni ya siku hiyo kuwa akipata hela ataelekea kwa baba
yake Chanika, sasa tulishangaa tu kikapita kimya hakurudi nyumbani kuaga
wala kuchukua nguo zake mpaka sasa tumesikia amekutwa amefariki dunia
bwawani,” alisema kwa uchungu mama huyo.
0 comments:
Post a Comment