Robin Williams akiwa na mke wake wa tatu, Susan Schneider.
Muigizaji
na mchekeshaji maaarufu wa Marekani, Robin Williams amejiua. Mwili
wake umekutwa nyumbani kwake California, Marekani Jumatatu Agosti 11,
2014.
Imeelezwa kuwa kwa siku za hivi karibuni Williams ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 63 alikuwa akipambana na sonona.
Muigizaji
huyo alikuwa hajitambui na hakuwa anapumua na hivyo kubainika kuwa
alijiua kwa kukosa hewa. Williams alionekana nyumbani kwake mara ya
mwisho mida ya nne usiku siku ya Jumapili.
Robin
alipelekwa rehab mwezi uliopita kujizuia kunywa pombe. Alikuwa
akihangaika kuacha kutumia cocaine na pombe katika miaka ya 80 lakini
hakuwahi kunywa kwa miaka 20.
0 comments:
Post a Comment